CHAMA KIKUU CHA UPINZANI CHADEMA KIMEENDELEA NA ZOEZI LA UCHAGUZI WA MABARAZA YAKE KATIKA SIKU ZA HIVI KALIBUNI HUKU WAKISUBIRI UCHAGUZI MKUU UNAO TARAJIA KUFANYIKA JANUARY 21.2025.
MABARAZA YOTE HIVI SASA YAMESHA MALIZA ZOEZI LA UCHAGUZI WA KUWAPATA VIONGOZI WAO WATAKAO WAONGOZA.
NA HATIMA ZA CHAGUZI HIZO ZILITAMATISHWA NA KUTANGAZWA KWA MATOKEO YA BARAZA ZOTE HUKU KWA UPANDE WA ANAWAKE (BAWACHA) ALIYEIBUKA MSHINDI NI SHARIFA SULEIMAN, BARAZA LA VIJANA BAVICHA LITAONGOZWA NA DEOGRATIAS MAHINYILA NA BARAZA LA WAZEE BAZECHA NAFASI IKICHUKULIWA NA SUZANI LYIMO
LENGO KUU LA UCHAGUZI WA MABARAZA HAYO KATIKA CHAMA CHA CHADEMA NI KUIMARISHA UONGOZI ILI KUENDELEZA DEMOKRASIA KATIKA CHAMA HICHO
BAADHI YA VIONGOZI WA NGAZI ZA JUU WAMEKUWA NA NA MAWAZO TOFAUTI TOFAUTI NA WENGINE WAKIDILIKI KUONESHA PANDE WANAZOEGEMEA KATIKA UCHAGUZI AMBAO UNATARAJIWA KUFANYIKA JANUARY 29 2025 HUKU WANAO WANIA NAFASI YA UWENYEKITI WA CHAMA HICHO NI FREEMANI MBOWE NA TUNDU LISSU.
MNAMO JANUARI 18 2025 JANUARI 19 MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI ULIANZA KUTIMUA VUMBI KATIKA MAKAO MAKUU YA NCHI JININI DODOMA HUKU MKUTANO HUO UKIWA NA LENGO LA KUMPATA MAKAMU MWENYE KITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFA
SIKU YAKWANZA YA MKUTANO HUO ILITOSHA KUMPATA MWENYEKITI WA CCM TAIFA NA WAJUMBE WA CHAMA HICHO KUWEZA KUMTAMBUA NA ALIYE IBUKA NA USHINDI NI STEVEN WASIRA.
WASIRA AMECHUKUA NAFASI HIYO MARA BAADA YA MTANGULIZI WAKE ABDULAHIMANI KINANA KUANDIKA BARUA YA KUJIUZULU KATIKA KITI HICHO
MNAMO JULAI 29,2024 KATIBU WA ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO WA CHAMA CHA MAPINDUZI NDUGU AMOS MAKALLA ALITHIBITISHA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA NA MWENYEKITI WA CCM TAIFA DOCTA SAMIA SULLUHU HASSANI KUWA AMERIDHIA OMBI LA KUJIUZULU KWA ALIYE KUWA MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA HICHO NDUGU ABDULAHMANI KINANA.
KUJIUZULU KWA ABDULAHIMANI KINNA KULISABABISHA CHAMA CHA MAPINDUZI KUKAA TAKRIBANI MIEZI SABA BILA KUPATA MRITHI WA KITI HICHO
WASIRA AMEWAHI KULITUMIKIA TAIFA KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA UONGOZI AKITUMIKA KAMA MKUU WA MKOA KWENYE MIKOA MBALI MBALI LAKINI MWAKA 1989 ALIHUDUMU KAMA WAZIRI WA KILIMO CHINI YA SERIKALI YA RAIS ALL HASSANI MWINYI.
