Samia Bara Mwinyi Visiwani

Bruno Kaitaba
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepitisha azimio la kumteua Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, Azimio hilo limepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM Mkoani Dodoma ambao ndiyo chombo cha mwisho cha maamuzi ya uteuzi wa mgombea wa tiketi ya urais kupitia chama hicho. Chama hicho pia kimempitisha Dkt. Hussein Mwinyi kugombea Urais kwa upande wa Tanzania Bara (Zanzibar). Uamuzi huo umefanyika mapema kuliko kawaida, na katika mkutano ambao awali haukupangwa kufanya maamuzi hayo katika ajenda zake. Mkutano huo ulikuwa na ajenda kuu moja ya kupitisha jina la Makamu wa Mwenyekiti (Bara) Rais Samia pia amemteua Katibu Mkuu wa CCM Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu, Nchimbi ni mwanasiasa mwandamizi na ameshika nafasi mbali mbali ndani ya CCM na serikali yake kwa miongo mitatu iliyopita.

Post a Comment

Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.